Je unadhani roho ya ukarimu / upole kwa wanawake juu ya wanaume umekufa au kupotea kabisa? Kwa jinsi wanaume wanavotenda na kuwa na matarajio makubwa siku hizi, ni dhahiri kwamba upole kwa wanawake 'unaweza' kuwa umetoweka.
Kwa baadhi ya wanaume, hii inaweza kuwa habari nzuri.Na kwa baadhi ya wanawake hii inaweza kuwa habari kuu kuwa roho ya kwao kwao haipo tena.
Ukarimu ji jambo jema na la kufurahisha.
Huchanganya kwenye uelewa , na kama utatumiwa na wawili wapendanao, hufanya maisha yao ya mapenzi kuwa mazuri sana.
Kama mwanamke natambua ni jinsi gani wanaume wengi hujaribu kuwa wakarimu wanapokua na wanawake.
Wanaume wengi japo hawapo hivyo hujitahidi sana mbele ya macho ya mwanamke waonekane wakarimu.
Kiukweli,
nimeona sana wanaume wengi wakiwafungulia wanawake zao milango aidha wa nyumba au gari, waingie au watoke, hii tu ni juhudi ya kudhihirisha ukarimu.
Hii sio common sana kwa wanaume wengi japo kwa America na nchi nyingine zilizoendelea huwa ni jambo la kawaida kwao.
Nili date na mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa ni mwanaharakati wa kupigania haki za wanawake(feminist). Alisema angependa wanawake wawe na haki sawa na wanaume na wakati wote alijaribu kuwafanya wanawake wajisikie kuwa wana nguvu sawa na wanaume. Nililipenda sana hilo wazo lake.
Lakini baadae nilikuja kugunua kuwa si mwanaue mkarimu.
Na sasa sihitaji mwanaume yeyote yule ninapokua mtaani eti anifungulie mlango wa gari. Na sitegemei kabisa anioeshe maigizo hayo kama vile mimi ni mtazamaji.
Nilimpenda yule mwanaume kwa siku ya kwanza, lakini baada ya pale nilikua nikimwona mwanaume mwingine akiwa anafanya yale matendo kwa mwanamke mwenzangu nilikua nikijisikia vibaya sana. Kwa sababu sikupenda jinsi mimi ilivyokkua nikifanyiwa. Nilipenda nijisikie wa kukubalika na kuheshimika na wa kupendwa, mwenye mtu anayenijali, na mwanaume ambaye angekua ananichukulia mimi ni sawa na yeye asingeweza kunifanyia haya yote.
[Soma: Mambo 10 yanayoharibu date na mwanamke wako!]
Wanaume hupenda kurahisisha kila kitu.
Ni kweli. Wanaume hupenda kufanya mambo yawe marahisi kadri wanavyoweza. Hawapendi kufanya mambo kuwa magumu, lakini wakati huo huo hawana tabia ya kuviheshimu vile wanavyovipenda kirahisirahisi.
Kama mwanamke atategemea mwanaume wake kuwa mkarimu, mwanaume mara nyingi hudhani mwanamke anahitaji yeye(mwanaume) awe mkarimu kupitiliza. Lakini kitu ambacho wanaume wengi hawakijui ni kwamba, ukarimu unaweza kuwa mojawapo ya kivutio kikubwa kwa mwanamke wakati wakifanya mambo mengine.
[Soma: Namna ambayo mwanaume anaweza kuwa mkarimu!]
Uzuri wa ukarimu huja wapi?!.
Wanawake hupenda kujisikia wanalindwa. Wanaume hupende kujisikia wanalinda.Ni jambo asilia. Mwanamke hujisikia mwenye furaha kama mwanaume atakayetoka naye out atamjali na kuonesha ishara ya kumlinda na kumthamini. Lakini pia, mwanaume hujisikia vizuri kama mwanamke aliyetoka naye out anaonesha ishara ya kumtegemea mwanaume kwa usalama wake na furaha yake.
Wakati waaume wengi wanalichukia wala la ukarimu, kitu ambacho hawakijui ni kwamba, wanafanya siku au mwenendo mzima wa dating kuwa mbovu na kufanya siku kuwa yenye kukera badala ya kufurahisha.
Kwa wanawake ambao hujishusha.
Kadri mwanamke anavyohama kutoka kwa mwanaume mbovu aliyekuwa naye zamani, huwa wanashangaa na kujiuliza kama yale mambo mazuri waliyokuwa wakiyasikia kama ni kweli au yalikuwa ya nadharia. Na mbaya zaidi, wanawake wengi hukata tamaa ya kuwa wakarimu na hivyo kuanza kuwa watukutu na hudumbukia katika wimbi la mapenzi ma mwanaume yeyote anayeonesha ishara ya kumjali.
[Soma:Kwanini nuksi zikutokee tu katika mapenzi?!]
Mage anaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Johnson, lakini, haufikiri kwamba anaweza kuwa na furaha zaidi akiwa na mwanaume mwingine? Anaweza kukata tamaa na ukarimu/upole wake kwa johson kupotea.
Na hiki ndicho hutokea sana kwa wanawake wengi. Huzishusha hadhi zao na kujiingiza katika mapenzi na mwanaume yeyote atakayeonesha ishara ya kumpenda na kumjali. Na hii inawafanya wanaume wengi ufikiri kuwa kila mwanamke anaweza kumpata kirahisi, na huchukia pale ambapo mwanamke anapenda amjali kwa heshima na adabu. Na hivyo, ukarimu kwa wanawake hupotea taratibu na uleta mkanganyiko tena kwa wanawake laini pia kwa wanaume kwa namna ya kuchukuliana katika uhusiano.
Lakini wapo wale wanawake ambao hujiingiza katika uhusiano kwa starehe ya muda mfupi hivyo wao huwa na furaha tu siku zote. Kwa wao ni ilimradisiku ipite, iwe mwanaume ni mkarimu au siyo mkarimu.[Soma:Ni wakati gani mwanamke humdanganya mwanaume kirahisi?!]
Aina mbili ya wanaume
Kuna wanaume ambao ni wakarimu na huishia kupata wanawake wakarimu. Lakini wapo wale ambao si wakarimu na huishia kuwaumiza wanawake wakarimu.Wanaume ambao huchagua na kutafuta mwanamke mzuri ambaye anaweza kudate naye au kutoka nae out mara nyingi hawanaga bahati hiyo. Kwa wao hujua tu jinsi ya kumhandle mwanamke. Kama mwanamke anategemea kuchukuliwa / kupendwa na mwanume wa aina hii, huwa ni rahisi sana kubebwa.
Kwa upande mwingine, mwanaume ambaye hujaribu kila wanaloweza kujizuia kuwa wakarimu, huishia kuwa na hasira. Huishia kufikiri wanawake huwachezea kihisia na kuwategea mitego. Hivyo hushindwa kujizuia na kujidhalilisha, na wakati huo huo, humpata wanamke ambaye anapenda mwanaume amjali lakini huyu mwanaume atamuendesha kama kituko na hatimaye huyu mwanamke atashindwa na kuachana naye.
[Soma: Ushauri ambao haufanikiwagi kwa baadhi ya watu!]
Hitimisho ni kwamba ukarimu hupotea pale unapouruhusu upotee!..
No comments:
Post a Comment