Thursday, March 30, 2017

Ishara 13 zinazoashiria anataka akuoe na anatamani kuishi na wewe!

 

Je kuna mwanaume anakuangalia sana kwa wakati mrefu ukiwa mgahawani, au darasani - au hata hotelini? Kuna mambo 13 atakayoashiria kuwa wewe ndiye mwanamke anayetaka kuishi na wewe.

Wanaume ni mojawapo ya viumbe vinavyochanganya sana duniani. Hiyo ni sana, na najua ni kweli. Wanaweza kukuonesha ishara zote na kila kitu kinaweza kikaonekana sawa, lakini wakati unataka kuenda katika hatua nyingine katika uhusiano wenu, wana
kukimbia taratibu kama mtoto anayetabaa.

Hii ishara inataka kuweka ukweli unaosema "ni vigumu kujua mwanaume anawaza nini". Na hauwezi kuwauliza kwa sababu wanaume wengi wanashindwa kujieleza namna wanavyojisikia kuhusu mwanamke. Hivyo unasemaje sasa? Namaanisha, je ni mimi mwenyewe ninayetamani wanaume waelewe kitu kinachoendelea vichwani mwetu kuhusu uhusiano wetu na wao?

Ishara za kuwa anataka kuoa na aishi maisha yote na wewe.

Ingawa wanaume hawasemagi kuhusu hisia zao, huwa wanatumia muda mwingi kukuonesha jinsi wanavyojisikia kuhusu wewe. Hufanya vitu vidogo vidogo hapa na pale ambavyo huashiria kuwa wanakujali na kuku-kubali!.

Kila mwanaume ni tofauti na kila mmoja ana njia zake za kukuonesha kuwa anakupenda na kukujali.

Lakini hizi ishara ya kwamba anataka kukuoa huwa zinafanana siku zote. Na hivi ndivyo utakavyojua kama anakufikiria wewe kama mke wake ajaye na anataka kukuvisha pete kwenye hako kakidole kako kadogo!..

[Soma: Mambo 12 ambayo hayavutii - Lakini ndiyo mambo halisi ya mwanaume unayetakiwa kuishi/ kuolewa nae!]

#1 Anakualika katika shughuli zote za familia yake(yao). Anapokualika ukutane na wazazi wake, marafiki zake, kaka na dada , na kukualika katika matukio yote ya familia yao, ni ishara kubwa ya kwamba anafikiri wewe ndiye chaguo lake. Tambua kwamba, hawezi kukutambulisha kwa kila mtu wake wa karibu na kukufanya uwajue kama hana lengo la kukufanya uwe mtu wake wa karibu zaidi katika maisha yake.

Labda anataka familia yake pia ikujue jinsi ulivyo na kitabia na namna unavyoshirikiana nao. Na hapo ndipo atakapojua kuwa wewe haumkidhi yeye tu, bali hata familia yake nzima.

#2 Anakuongelea na kukusifia wewe kwa wengine. Ulishawahi kumfuma anaongea na wenzake kuhusu wewe, au kwa familia, au wafanyakazi wenzake? Hizi sifa sio za kuzichukulia kirahisi tu. Kama mwanaume anaweza kukusifia kwa watu wake wa karibu, inamana ametambua uwepo wako na jinsi ulivyo wa thamani kwake - hii inamaanisha unamfaa.

Akikuona anaona utimilifu wake - kwa maneno mengine bila wewe hajakamilika, na akiwa anakuongelea anajisikia furaha pia. Hii inamaanisha anakuona wewe kama sehemu ya maisha yake - kitu ambacho ni ishara kubwa kuwa amekupebda kuliko wote na anataka muishi pamoja.

#3 Anaongelea kuhusu mipango ya baadaye akikuhusisha katika hiyo mipango. Simanishi kupanga mipango ya mtoko wa weekend inayokuja - Hapana. Naongelea kuhusu mipango ya miaka ijayo. Kama anakuweka katika malengo yake ya baadae, hii inamaanisha amepanga kukuweka karibu yake kwa muda mrefu. [Soma: Ishara 14 zisiofichika kuwa anataka aishi maisha yake yote na wewe!]

#4 Anataka kuishi na wewe. Wanaume hupenda sana sehemu wanayoishi. Kwa hiyo kama anaongelea jambo la wewe ukakae naye, kitu anachojaribu kukisema hapo ni kwamba anataka kuishi na wewe katika maisha yake.

Wanaume wengi wakiwa kwenye uhusiano hawapendi kuishi na mwanamke - hupenda aje akae siku moja au mbili aondoke. Anapo jifunga na kuamua kuhitaji kuishi na wewe, katika mawazo yao wanakuwa na pete tayari usubiri kuvishwa tu.

#5 Mkiwa mnaongelea kuhusu watoto. Kitu ambacho mwanaume anakipenda akiwa kwake ni - Uhuru + Uhuru wa muda(Free time). Na ujue hauwezi kuwa free kama mna watoto. Lakini kama nyie wawili mtaongelea kuhusu watoto wenu wa baadae, anakuona wewe kama mama yao na mke wake. Na ni ishara kubwa sana kuwa anataka kuishi na wewe.

#6 Mara nyingi atakua anaongea neno "sisi" au "tuta" akiwa anaongea na wewe au wenzake. Akiwa na wewe kwenye group, je anaongelea jinsi "sisi/tuli-enda..." na "tuka..." ...enda kuangalia ile move? Kama anaongea na kuweka maneno kama "Nime" badala ya "tume" anakuona wewe kama bidhaa yake tu.

Akiwa anakujumuisha katika maongezi yake, inamaanisha anatambua uwepo wako na anaona kama wewe na yeye ni kitu kimoja ambacho ndoa inapaswa kukibariki. Kwa maneno mengine: Anataka akuoe na muishi maisha yote pamoja kama mume na mke!.

#7 Je anakasirika na kunung'unika mialiko ya harusi inavyokuja?. Wanaume wengi ambao hawana kabisa wazo la doa akilini mwao utawasikia waki lalamka, nung'unika kuwa mialiko imekuwa mingi kwake.

Lakini kama hajakasirika a anafurahi na anatamani kushuhudia hiyo harusi, inamaanisha amefikia hatua anayofurahia hilo tendo na yeye anatazamia wa kumpata wa aina yake ambaye watu  watahhudhuria katika sherehe yake. [Soma: Ishara 25 zinazoashiria una homa ya Ndoa/Harusi!]

#8 Yupo wazi kuhusu kila kitu kwako. Uaminifu na uwazi ni ufunguo mkuu wa nyumba ya mahusiano. Kama anaweza akakueleza maungufu yake, mambo yake ya kikazi, au mengine yoyote yanayomuhusu ambayo si kawaida kuyasema kwa kila mtu, ujue anakuona mtu wa thamani ambaye anaweza kumvisha pete.

#9 Anathamini mawazo yako katika mambo makubwa. Hili ni jambo kubwa sana. Kama kabla haja enda shopping au kwenda kununua gari , ana anataka mawazo yako juu ya jambo hilo kabla hajalifanyia kazi, Hii ni ishara kubwa kuwa anakuheshimu kama mtu muhimu usiyeweza kumshauri kitu kibaya hivyo unafaa kuihi naye.

Anafanya hivyo kwa sababu anajua nyie wawili mnaweza kuwa kitu kikubwa, na kufanya maamuzi juu ya mambo mengi ya msingi. Hii ni ishara kubwa ya kuwa una malengo(future) na mtu fulani. [Soma: Ishara 11 za kuwa mwanaume unaye toka naye - Ndiye!]

#10 Mnatoka wote kipindi chake cha likizo. Muda wa likizo ni muda mzuri kwa mwanaume kuwa mbali na kazi na masumbuko mengine ya maisha. Kama atakwenda na wewe popote iwe hata mbugani, hii ni ishara kubwa kuwa unaweza kumsahaulisha matatizo yote ya kazini. Na hii ni ishara ya kwamba anataka kuishi nawewe.

#11 Siku zote anapenda kusuluhisha mgogoro kati yenu kama upo. Kama mwanaume hataki kuwa na wewe katika maisha yake, basi ukitokea mgogoro kati yenu hatapenda kuusuluhisha. Wao hunyamaza tu mpaka pale mambo yatakapoonekana sawa - au wewe umejiondosha mwenyewe.
Lakini kama mwanaume wako anajaribu kusuluhisha mgogoro wowote mlionao kwa wakati huo, hii inamaanisha anataka kuhakikisha mnaendelea kuwa pamoja kwa amani - na ni ishra kwamba hataki kukupoteza na anataka muishi wote.

#13 He tells you. If he tells you that he wants to marry you someday, or that you’re the one for him, then that’s the only sign you need! When this happens, he’s certain he wants to marry and spend his life with you.y

#12 "Anajisikia" kuwa na hilo wazo - la kuoana. Je alishawahi hata kugusia hio jambo mnapokuwa katika maongezi yenu ya kawaida? Kama ni ndiyo, atakuwa anawaza kama wewe utakubali kuishi naye. Kuongelea kuhusu ndoa kwa mwanaume yeyote ni ishu kubwa, na kama anajisikia kuongea kuhusu ilo pamoja na wewe, andaa kidole maana muda si mwingi atakuvisha pete.[Soma: Jinsi ya kumshawishi akuvishe pete kwa kumsoma mawazo yake!]

#13 Atakuambia. Kama atakuambia anataka akuoe muda mfupi ujao, au wewe ni chaguo lake, sasa hiyo ndiyo ishara pekee ya mwisho atakayokuonesha! Hili likitokea, Ujue hilo ndo wazo lake la mwiho kwako.

[Soma: Ishara 25 za kwamba mwanaume anakupenda kupitiliza lakini anashindwa kukuambia]

Kujaribu kugundua mwanaume anawaza nini siyo kitu rahisi. Ukiona hizi ishara 13 kaza waya pete ipo njiani inakuja kwa ajili yako, na utajua wewe ndie wa pekee kwake!..

No comments:

Post a Comment