Monday, January 16, 2017

Vitu 25 vinavyomfanya mwanaume kuwa na mvuto kwa mwanamke

Ni kitu gani mwanamke anakuta ni cha kuvutia sana kwa mwanaume?

Kama hauji basi hapa utapata kufahamu, list ya vitu 25 itakueleza kila kitu unachotaka kuju kuhusu wanawake wanapenda nini na wanachukia nini!.

Wanaume siku zote wanavutia kwa wanawake, mathalan wacheza mpira wa miguu(footballers) wakiwa na sixpack nywele wamenyoa vizuri au kuziweka kwa mitindo yao na vingine vingi. Ingawa, mara nyingi wanaume kama hao huonekana tu wazuri kwa nje, Lakini baadhi yao ndani huwa hawana kitu.
Amini usiamini mapenzi sio kitu pekee kinachomfanya mwanaume kuwa na mvuto. Lakini hata iweje,

tips 25 inahusisha mambo mwanawake anayopenda sana kuyaona kwa mwanaume na kumvutia.
#1 Mwanaume mwenye malengo. Haijalishi ni malengo ya aina gani, iwe malengo yanayohusiana na kazi yako au kusaidia jamii baada ya muda wa kazo au malengo yoyote yale, mwanaume anayekua na malengo na nia ya dhati ya kufikia malengo yake, huwa na mvuto wa ajabu sana kwa mwanamke wa aina yeyote.

#2 Mwanaume mwenye uwezo wa kusuluhisha mambo. Haimaanishi kwamba inatakiwa tuwe wajuaji wa kila kitu, hapana mana mwanamke huchukia mwanaume wa aina hiyo, ninacho maanisha ni kwamba, mwanamke anapokua na uwezo wa kusuluhisha mambo huwa na mvuto wa aina yake, hata kama hali yake ya kiuchumi sio kubwa sana. Mwanamke unatakiwa kuwa na uwezo wa kusuluhisha mambo magumu yanayokukabili au kumkabili mwenzako au hata jamii. [Soma: Mambo 20 unayoyahitaji kuwa mwanaume wa kweli]

#3 Mwanaume anayeijali familia yake. Mwanaume anayekubali kuwajibika na kuijali na kuithamini familia yake - eidha wawe wazazi, watoto, kaka au dada, au hata ndugu - inaonesha ukubwa wa fikra na upendo, na vyote hivyo huwa na mvuto.

#4 Mikono ya mwanaume. Labda ni kwasababu inaweza kutengeneza, kuumba, na kutekeleza ubunifu mwingi

#5 Mwanaume mwenye ndoto kubwa, na anaezifuata. Ndoto ni kitu kikubwa katika maisha endapo mtu anataka kufanya kitu katika hii dunia kwa utofauti ili awe mtu. Hakuna kitu cha kuvutia kama mwanaume anayetambua anataka nini katika maisha yake, na kukifanikisha huku akiwa bado na usongo(passion).

#6 Mwanaume wa viwango. Upole kwa mwanamke sio kifo. Mwanaume mwenye viwango - "sio swaga" - ni kama dhahabu. Fungua mlango, vaa boxa au bukta, na umwambie mwanamke wako ni jisni gani alivyo mrembo na anavyokuvutia kila muda. [Soma: Upole kwa mwanamke umekufa kwa sababu mwanaume ni mvivu]

#7 Mwanaume asiyeogopa kumueleza mwanamke ni jinsi gani anavyojisikia kuhusu yeye(mwanamke). Mwanamke hapendi sana mtu imara tu, mkimya - inakera sana na nivigumu kumfurahia mtu wa hivyo. Kitu ambacho mwanamke kitampa wendawazimu juu ya mwanaume, ni mwanaume ambaye ambaye anaweza kuniambia anajisikia vipi kuhusu mimi na anahitaji nini kutoka kwangu, na hisia zake juu yangu. [Soma: Pillow talk - Maongezi nane ya kitandani ambayo yatamfanya akupende sana]

#8 Mwanaume anaye tufurahisha kitandani. Mwanamke hujisikia sana furaha endapo mwanaume wake anaweza kumfurahisha kitandani. Mwanaume wa kweli huwa haarakishi mambo, kuvua nguo tu na kuanza shughuli. Tumia muda mwingi kupita naye engo zote za mwili wake na uhakikishe anafurahi sana hata kabla hamjaanza kufanya mambo. Hakikisha anaridhika kabla hajalala.[Soma: Vitu 12 ambavyo wanaume wengi sana huvifanya kitandani ambavyo huwafanya wanawake kuigiza wameridhika!.]

#9 Mwanaume mwenye mpangilio. Anayejua jinsi ya kumfata mkubwa wake(boss), kuwa na tabia njema kwa wazazi na wanajamii, na kula vizuri ni vitu vikubwa sana kwa mwanamke.

#10 Mwanaume mwenye kujiamini, lakini sio mwenye sifa za kuzidi. Confidence ni kitu kikubwa sana ambacho mwanaume yeyote anapaswa kuwa nacho, Lakini mwanaume mwenye tabia ya woga ni aibu kwake. Mwanaume anayejijua kuwa anaujuzi juu ya jambo fulani, alafu haoni ulazima sana wakujitangaza bila sababu ndiye anayechukua points kubwa kwa mwanamke.

#11 Mwanaume anayependa kucheka(kistaarabu), na kutabasamu humfanya mwanamke pia kufurahi na kucheka. Kicheko kimethibitishwa kuwa mojawapo ya vitu vinavyomfanya binadamu aongeze siku zake za kuishi, tena maisha ya furaha. Kama mwanaume anaweza kumfanya mwanamke wake kucheka, na wakacheka wote kwa pamoja, hiyo ni ushindi mara mbili(double win). [Soma:Vitu mwanaume anavyoweza kufanya , vikamchekesha(kumfurahisha) mwanamke yeyote yule na kukupenda kupitia hilo]

#12 Mwanaume anayekubali makosa pale anapokosea. Naongelea makosa madogo madogo kama kutotakiana siku njema, na makosa makubwa kama kusahau birthday ya mwanamke wako. Kama mwanaume anaweza kuyakubali makosa yake na kuomba msamaha kwa sababu naye pia ni binadamu. Mwanamkke HATACHOMOKA.

#13 Mwanaume ambaye ni mwerevu wa akili(Intelligent). Kuwa na PHD sio kitu, lakini mwanaume anayeweza kuisimamia mada yeyote anayoipenda, inavutia sana. Pia vitabu vya kusoma chumbani kwa mwanaume humuongezea sana point.

#14 Mwanaume asiyeogopa kujiwekea kiapo(Commitment). Wanawake huchukia sana na huchoka kusikia kwamba sababu hatuwezi kuwa na mahusiano bora zaidi ni kwasababu wanaume huogopa kuweka viapo kwa wapenzi wao. Huo ni Ulofa. Mwanaume asiyeogopa kusema "Ndio/Yes, nitakua wako, na ninakuahidi nitakua wako mpaka hapo tutakapo amua vinginevyo" humpagawisha sana mwanamke. [Soma: Mambo 10 yanayokufanya uwe na uoga wa kuweka ahadi].

#15 Mwanaume anayeweza kutu shangaza(Suprise Us). Hii sio tu suprise siku ya birthday ya mpenzi wako au kuja nyumbani na maua(flowers), HAPANA. Hii inamaanisha kufanya vitu vipya sehemu yoyoote ile ambayo itatufanya sisi tujisikie kama unaweza kufanya kitu chochote wakati wowote.

#16 Mwanaume anayeweza kupika. Kumpikia na kumlisha mwanamke itakua kama mtu anayeendesha gari na kukanyaga mafuta kwa speed kubwa, utamteka mwanamke kwa kipindi kifupi sana. Kama unaweza kumpikia mwanamke chakula kitamu, hatakua na la kusita kuhusu wewe, mana itamfana ajione wa kipekee na mwenye kupendwa.

#17 Mwanaume ambaye ni baba mzuri. Kuwa mzazi uwa inagarimu muda mara nyingi pamoja na nguvu, kama mwanaume unaweza kumbadilishia mtoto nguo anapokua amejikojolea, kumlisha chakula, kucheza na mtoto, kumbembeleza mpaka alale, utamfanya mwanamke wako awe na kichwa kikubwa mara 3 kwa kujisifu ana mume mzuri.

#18 Mwanaume anayeweza kututia moyo(Motivation). Kumtia mtu moyo mara nyingine uwa ni kitu kigumu pale maisha yanapokwenda kombo na unahisi hauna pakutokea. Maisha ni kisomo kisichoisha, kila siku tunajifunza vitu vipya na ambavyo vinaweza kubadilisha sura ya maisha yetu wakati wowote kama tuna nia. Mwanaume anayeweza kututia moyo katika mambo ambayo tunaona ndo mwisho wetu, huyo mwanaume ni zaidi ya mwanaume.

#19 Mwanaume asiyeogopa kukua/kujifunza. Mtu hatakiwi kusitisha zoezi la kujikuza kiakili na kitabia katika dunia tunayoishi. Hakuna mtu anayejua kila kitu, ila tunajitahidi kila siku kuwa na vitu ambavyo vinaweza kutufanya sisi tuwe bora zaidi kadri siku ziendavyo. Mwanaume anayependa kujifunza na kama dhahabu kwetu sisi wanawake.

#20 Mwanaume anayeweza kumudu udhaifu wake. Kuelezea tamthilia nnzima kwa kichwa, au kuwa addicted na movie au games sio kitu kibaya, ilimradi tu visiwe va kuzidi mpaka kukera. Cha muhimu ni kwamba muda wako mwingi usiishie huko kiasi kwamba ukasahau kufanya mambo mengine ya muhimu.

#21 Mwanaume anayeweza kukumbatia. Kukumbatiwa inamfanya mwanamke kujisikia analindwa, anapendwa, unamjali, na ni ishara ya upendo , ni mambo yanayotfanya kujiamini na kujiona wa kipekee sana duniani. Kama mwanaume anaweza kufanya hivyo bila woga, lazima aiteke akili ya mwanamke wake.

#22 Mwanaue asiyeogopa/ kuona aibu kutoa nje chombo cha takataka/uchafu. Wanaume wengi hawapendi kutoa uchafu nje kwa kuhisi kwamba wataonekana wanamilikiwa au kuendeshwa na mwanamke wake. Hili sio kweli, mwanaume anayeweza kutoa takataka nje, anayafanya maisha ndani ya nyumba yake yawe yamekamilika, yenye furaha. Vitu hivi uonekana vidogo lakini kwa mwanamke vina maana kubwa sana. Kama mwanaume anaweza kumsaidia mwanamke wake vikazi vidogo kama kuosha vyombo, au kudeki, au kupasi na kupanga nguo kwa mda mchache alionao,inamfanya mwanamke aone unawajibika, na hautamvutia tu mwanamke wako, lakini hata marafiki zake.

#23 Mwanaume ambaye tunaweza kucheza nae. Maisha hayatiki kuwa ya misongo ya mawazo kila wakati, wakati mwingine unatakiwa kuwa na muda wa kucheza na kufurahia penzi lenu wewe na mwanamke wako. Sisi tunapenda raha, kwa hiyo kama mwanaume anaweza kutufanya tufurahi muda wote, inatufanya tuwaone wamekamilika. [Soma: Mambo 50 afanyayo mwanaume ambayo wanawake hupenda].

#24 Mwanaume anayependa mazingira. Sisi ni sehemu ya mazingira, na mwanaume anayelitambua hili na kuyajali mazingira yanayomzunguka kwa kuyafanya safi na ya kuvutia, huchukua nafasi kubwa sana mioyoni mwetu.

#25 Mwanaume awezaye kutupenda sisi tulivyo. Mwanamke anatakiwa kushighulikia mambo ambayo yanamfanya yeye asiwe mwenye kujiamini(confortable), tunahitaji mwanaume mwene uwezo wa kutuambia badilisha kitu X, Y, Z. Mwanaume anayempenda mwanamke jinsi alivyo, na sio aonekanavyo, au anafanya kazi gani ni mwema siku zote. [Soma: Tabia 12 za mashujaa zinazozomfana mwanamke kupagawa!]

Kuwa na Sexy body sio kitu pekee kinachoweza kumvutia mwanamke. Jinsi mwanaume anavyo ishi na kutenda na mitazamo yake ya kifikra na moyo wake ndivyo silaha pekee ya kumuangamiza mwanamke.

[Soma: Vitu 50 vya kumuambia mwanamke unayemtaka/kumpenda]

Kwa hiyo next time ukiona mwanamke hasomeki au hakuelewi, tilia maanani haya mambo 25 na muda sio mrefu atakua wako. Itakufanya wewe uwe wa tofauti.

4 comments:

  1. Ushuhuda

    Nilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
    Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
    Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.

    Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:

    ✅ Maneno ya mapenzi
    ✅ Tahadhari za Ujauzito
    ✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
    ✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.

    📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
    📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159

    Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!

    ReplyDelete